Mshukiwa Wa Mauji Ajisalimisha kwa polisi Baada Ya Kujificha Kwa Miezi 2

Mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka arobaini anayetuhumiwa kumuua nduguye mwezi wa tano mwaka huu amejisalimisha kwa maafisa wa polisi wa Busia.

OCPD  Masai Makau amesema mshukiwa  Samuel Wabwire amekuwa akijificha mjini Busia akihofia kuuwawa na wananchi tangu amuue nduguye  Wilfred Egesa Wabwire mwishoni mwa mwezi wa tano.Makau amesema mshukiwa huyo atafikishwa mahakamani mapema juma lijalo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kiakili.