Msichana, 17, auawa na mwili kutupwa katika shamba la mahindi

Msichana wa miaka 17 auwawa na mwili wake kutupwa katika shamba la mahindi karibu na maeneo ya Kipkaren, Eldoret.

Polisi wanakisia kuwa mwanamke huyo alinajisiwa na kuuliwa katika shamba hilo. Wiki iliyopita mwili wa mwalimu wa shule ya upili ya Ngeria eneo hilo pia ulipatikana katika shamba la mahindi.

Wakazi wa KIpkaren wakiongozwa na Paul Kibor wamewasihi polisi kuhamasisha msako wao karika maeneo ambayo majambazi hutumia mashamba ya mahindi kama maficho yao.

Kwingineko, kaunti ya Taita Taveta imewaahidi wafanyikazi wanaogoma kuwa itaanza kuwalipa mishahara yao hii leo.

Akihutubia wafanyikazi walioandamana hadi afisi ya gavana, kaimu waziri wa fedha Davis Mwangoma amesema kaunti hiyo imekuwa na changamoto ya kulipa mishahara baada ya kucheleweshwa kwa mgao wa fedha za kaunti kwani ushuru unaokusanywa ni mchache mno kulipia mishahara.
Wafanyikazi hao walisusia kazi Leo na kukwamisha huduma katika idara mbalimbali za kaunti.

-Mathews Ndanyi