Msichana afukuzwa kanisani baada ya kushiriki mapenzi na mwanamziki

Mwezi uliopita, mwanamziki maarufu humu nchini alidaiwa kutokuwa mwaminifu ndani ya ndoa yake huku mkewe akisema kuwa mwanamziki huyo alishiriki ngono na msichana mdogo.

Kulingana na msichana aliyehuskia, yeye alikuwa kwenye harakati za kutafta ushauri jinsi ya kuiendeleza taaluma yake ya uigizaji ndiposa akapatana na mwanamziki huyu aliye mwalika nyumbani kwake na kisha kumlazimisha kushiriki naye ngono.

Kulingana na vyombo vya karibu, inasemekana kuwa msichana huyo ameondolewa katika nafasi ya kuwakaribisha wakristo ndani ya kanisa alilokuwa akishiriki ibada yake ya misa kwa mwaka mmoja sasa.

Viongozi wa kanisa hilo wanasemakana kuchukua hatua hio ili kuwakinga mastaa wao wanaoshiriki kanisa hilo.