Msichana apata mimba ya babake na kumpokonya mamake mume

lady
lady
Kuna Vitu ambavyo hufanyika wakati mwingine  na kukufanya hata uumwe na kichwa kwa sababu huwezi kuelewa mbona vinafanyika na kwa nini wahusika wana ujasiri wa kufanya vitendo kama hivyo .

Sio jambo  linalokubalika kwa watu wenye uhusiano wa damu kuoana au hata kushiriki mapenzi ,lakini kuna watu ambao huvnja mipaka hiyo na kutenda mambo yasioweza kueleweka . Loise*  yupo hospitalini sasa baada ya kurukwa na akili wakati alipogundua kwamba binti yake  wa kwanza ,anaishi na babake  wa kumzaa kama mume na mke Nairobi . Mwanzo  anasimulia jinsi hali hiyo ilivyofika hatua ya yeye kulazwa hospitalini na masimulizi yake yanaenda hivi .

Binti yake Loise alikuwa akisoma katika chuo kimoja ,eneo la Thika  , kila siku alikuwa akipanda gari hadi katika eneo la muthurwa ambako aliishi katika  nyumba moja na babake .Babake  amestaafu kutoka shirika moja la serikali   na alikuwa akingoja kupewa malipo yake ya kustaafu  Shirika  alilokuwa akilifanyia kazi lilimpa nyumba ya kuishi akingoja kupewa malipo yake na Mzee alikataa kurejea nyumbani mashambani lakini mkewe ,Loise aliamua kurudi nyumbani . Wakati  Mume wake Loise alipoamua kuishi jijini ili kungoja malipo yake ya kustaafu ndipo binti yao mkubwa alipojiunga na chuo chamafunzo ya ushonaji Thika ,na hapo ndipo ngoma ilianza kudhihirika . Kumbe baba na binti yake walikuwa wakishiriki mapenzi ,licha ya kujua kwamba vitendo vyao sio sawa . Watu ambao hawakuwa wamewajua ,walifikiri kwamba ni mtu na mumewe na wakashangaa mzee aliweza vipi kumuoa msichana mdogo ,wasijue kwamba ni baba na mwanawe!

Yote yaligunduliwa wakati nyumba za shirika alilokuwaakilifanyia kazi mzee zilipobomolewa ili kuunda soko la muthurwa.  Mzee alikataa kwenda mashambani na mke wake akaanza kujiuliuza maswali .Alifahamu kwamba binti yao alikuwa akiishi na babake lakini hakuwahi kufikiria kwamba kuna maovu yaliyokuwa yakifanyaka  katika nyumba ile . Kama kila siri kubwa ambayo hulindwa na nguvu zote kwa sababu kila siri ni nzito ,walizidiwa na mizgo wa kuificha ile siri wakati binti yao alipopata mimba . Mzee hakusema lolote ,na Loise alishangaa mbona mume wake hakuwa na ukali kwamba binti yao alikuwa amepata mimba ilhali alikuwa shuleni .

Siku moja ,baada ya  mtu na babake kuhamia mtaa mwingine wakati nyumba yao ilipobomolewa ,Loise aliamua kuja jijini ili kufahamu walikokuwa wakiishi na mbona mzee wake hakuwa akitaka kuja nyumbani . Akiuliziaulizia kuhusu nyumba ya mume wake ,majirani walimuambia kwamba mzee na mke wake wanishi katika nyumba fulani na akaonyeshwa . Loise alishangaa mbona majirani walikuwa wakimuambua kwamba mume wake alikuwa na mke ilhali alikuwa akiishi na binti yao. Baadaye  wakati jioni ,Mzee alikuja na akafungua mlango ,Loise amesema kwamba amefunga safari ya kuja Nairobi na hivyo basi mume wake alikuwa mkali na hata alisita kumkaribisha katika chumba . Binti yake aliingia muda mfupi baadaye huku mimba yake ikiwa sasa imeanza kuonekana . Loise alipoingia katik kile chumba aliona tu kitanda kimoja na  viti vya plastiki.Alimuuliza mumewe ni wapi binti yao alikuwa akilala kwa sababu haoni chumba cha pili au hata godoro lake mle chumbani .Mzee hakumjibu na Loise akakumbuka alichoambiwa na majirani kwamba mzee na mkewe wanaoshi katika ile nyumba .

Hofu yake iligeuka kuwa zimwi la fikra ambazo kila siku anataka kusahau .Binti yake alipofika chumbani ,alimsalimia mamake na kisha akaketi na babake pale kitandani .Walivyoangaliana sio kama inavyofaa mtu na babake kuangaliana na pale pale ,Loise alijua kwamba yamemfika masaibu ambayo hatoweza kujikwamua kwa njia rahisi . Wote walimuangalia machoni na kumuambia kwamba  mimba ile ile ya mume wake-kwa ufupi ,baba alikuwa amempa mimba binti yake na  kwa maksudi . Hapo ndipo Loise alipozirai na kujipata hospitalini kisha baadaye katika kituo cha usaidizi wa kisaikolojia .Mengine ni historia .