Msichana wa 11 kunajisiwa katika kaunti ya Samburu

pitypglgt9psvo6o45bb5cb8bc78ab
pitypglgt9psvo6o45bb5cb8bc78ab
Msichana wa miaka 11, wa darasa la kwanza kutoka eneo la Loosuk kaunti ya Samburu anaendelea kupona katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya Samburu, baada ya kunajisiwa na mtu ambaye anajulikana mzuri na familia yake.

Msichana huyo anapokea matibabu baada ya kupata majeraha wakati alipokuwa akinajisiwa, mratibu wa matibabu katika hospitali hiyo Silas Lodokei alisema kuwa msichana huyo aliweza kutibiwa na madaktari na kwa sasa yuko katika hali nzuri.

"Mgonjwa aliletwa, tulimwangalia kisha tuka mpeleka katika ukumbi (theatre) kwa sababu alikuwa amepasuka sehemu yake ya siri,

"Tuliweza kumtibu na sasa yuko sawa na yuko katika wadi na hali yake ni nzuri." Alieleza Silas.

Chifu wa eneo la Marala Selina Lemakara  aliweza kukejeli kisa hicho, na kusema kuwa mshukiwa wa kitendo hicho anafahamika kwa sana katika eneo hili.

Aliongeza na kusema kuwa alitoroka baada ya kufanya kitendo hicho siku ya Jumatatu.

"Nitafuatilia mshukiwa huyo ni hakikishe kuwa amekamatwa na ameshtakiwa na kisha ameenda jela kwa ajili ya kitendo hicho." Aliongea Selina.

Lemakara na mwenye kiti wa nyumba kumi wa eneo hilo Solomon Wanyeki waliwaimiza wanaume wa kaunti waweze kuwatafuta wanawake ambao wamekomaa kuliko kuwaaribia wasichana wadogo maisha.

Ni maneno ambayo yaliungwa mkono na mdogo wa mwenyekiti wa nyumba kumi Gulleid Mohammed na kuiambia serikali kuwa wasiweze kumuhurumia mshukiwa huyo.

"Ni jambo la aibu sana kwa msichana mdogo kama huyo kunajisiwa, mshukiwa huyo hapaswi kuonyeshwa huruma na anapaswa kufungwa jela kwa zaidi ya  miaka 20." Mohammed alizungumza.

Aliweza kuwaomba na kuwauliza wazazi wawe macho na kuwalinda watoto wao vizuri ili kisa kingine ikama hicho kisiweze kutokea.

Bwana Wanyeki aliweza kefyakefya wakazi wa eneo hilo dhidi ya kuwajibika katika wito wa kutatua kisa cha kunajisiwa nyumbani na kuwaambia kuwa hiyo ni kuwanyima watoto haki yao.

"Jambo kama hili halipaswi kutatuliwa nyumbani, unapata kisa kama hiki kimetendeka alafu watu wanatatulia nyumbani na kupeana haki." Wanyeki alieleza.