Msichana wa miaka 13 aapa kelea mimba ya babuye

Yatima mwenye umri wa miaka 13, aliyenajisiwa na babuye na sasa ana mimba ya miezi mitatu amesema hataitoa mimba kwa kuhofia maisha yake.

Amina, (ambalo sio jina lake halisi) ameambia gazeti la The Star katika mahojiano ya kipekee kwamba amekuwa akinajisiwa na babuye kwa miaka minne iliyopita.

Msichana huyo alifichua kwamba babuye angemshukuru sana, kila alipomaliza kumnajisi na kumshawishi kwa shilingi elfu moja ili asaliye kimya.

“Niliambiwa na familia yangu kwamba nitafariki ikiwa nitajaribu kuavya mimba yangu. Kwa hivyo nitakaa nayo,” alisema.

Mshukiwa, Suleiman Hussein alikamatwa mtaani Kibera Jumanne usiku wiki iliyopita na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Kilimani.

Siku ya Ijumaa, mhubiri huyo wa Kiislamu alifikishwa mbele ya hakimu mkuu mkaazi wa Kibera Esther Boke na kushtakiwa kwa kosa la kunajisi.

Pia alishtakiwa kwa kosa la kushika msichana huyo mdogo sehemu zake za siri.

Mahakama ilidinda kukubali ombi lake kuachiliwa kwa dhamana, kwa misingi kwamba huenda angehitilafiana na ushahidi kutokana na wadhifa wake katika jamii.

Hospitali ya Nairobi Women ilithibitisha kwamba mwathiriwa alikuwa na mimba ya miezi mitatu.