Miongoni mwa viongozi waliomkaribisha Ruto na kuapa kumuunga mkono katika uchaguzi mkuu ujao ni pamoja na naibu gavana wa Kisii Joash Maangi ,wabunge Silvanus Osoro (South Mugirango) na Alpha Miruka (Bomachoge Chache). Siku ya jumamosi kulikuwa na rabsha katika mkutano wa BBI huko Kituo ambapo baadhi ya washirika wa Naibu wa rais walihangaishwa na watoa ulinzi pamoja na baadhi ya waliohudhuria mkutano huo.
Wabunge waliowasili baada ya mkutano huo kuanza walizuiwa kufika jukwani ambapo kiongozi wa ODM Raila Odinga alimywa ameketi pamoja na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka ,magavana na viongozi wengine walioachaguliwa . Zaidi watu 40 wa kutoa ulinzi waliwavizia na kuwazuia viongozi wa tanga tanga wakiwemo Kipchumba Murkomen (Elgeyo Marakwet) na seneta wa Kericho Aaron Cheruiyot dhidi ya kufika jukwani . Moses Kuria pia aliyapitia masaibu kama hayo alipofurushwa kutoka mkutano huo .