‘Msiniliake katika harusi zenu’-Bien wa Sauti sol awaambia rafiki zake waliokosa  kualikwa

Bien
Bien
Msanii wa kundi la muziki la Sauti Sol  Bien aime Barza  alifunga ndoa na mpenzi wake Chiki Onwukwe,  katika harusi iliyokuwa ya waalikwa pekee mtaani lavington katika eneo la Pallet Cafe, Lavington,  ijumaa wiki jana .Bien  amesema hakuweza kuwaalika rafiki zake wote nkwa sababu harusi yake ilipangwa kuwahusisha watu wa familia na rafiki wa karibu ‘ni kwa wale wanaonifahamu kama Alusa sio Bien’”amesema msanii huyo.

Baadhi ya rafiki zake hawajafurahi baada ya kuachwa nje ya orodha ya wageni walioalikwa katika harusi hiyo . Lakini Bien hana cha kumpa wasia wasikwa sababu harusi ilikuwa yake na hakuna anayeweza kudai kuwa na haki ya kuhudhuria harusi ambayo hajapewa mualiko .

" Sina haja ya kuhudhuria harusi kwa sababu nimeenda katika harusi  nyingi.Ilikuwa njia yangu ya kuadhimisha kujitolea kwangu kwa mke wangu’ amesema  Bien .

Bien amewashauri wanaopanga kufanya harusi kuhakikisha kwamba wanaanda hafla  wanazoweza kugharamia kwa urahisi ."Harusi ni mwanzo wa maisha yako .kwa hivyo usitumie pesa zakozote kufanya harusi .Fanya kitu unachoweza kugharamia .Hakikisha unatumia pesa nyingi katika fungate yako kuliko unazotumia katika harusi yako’ amesema Bien . Bien alitumia kiasi kisichozidi shilingi laki tatu katika harusi yake .Bien na Mke wake  hawajaenda honeymoon kwa sababu ya mkurupuko wa virusivya Corona