Msomaji habari Ann Kiguta asimulia uhusiano wake na marehemu Daniel Chemjor

Mwanahabari Ann Kiguta amesimulia kwa majonzi jinsi alivyokutana na marehemu Daniel Chemjor.

Ann alikuwa anamuomboleza Daniel aliyefariki dunia baada ya kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani katika mto wa Kerio .

Daniel Chemjor ambaye ndiye mwendesha vipindi runinga ya K24 aliaga dunia wakati na ambapo gari lake lilitumbukia mto Kerio kwenye barabara ya Iten – Kabarnet.

https://www.instagram.com/p/B5NQwI7hkDY/

Ajali hiyo ilitokea usiku wa Jumatano ambapo anasemekana alikuwa safarini kumwona mkewe aliyekuwa amejifungua.

Ann alikutana na marehemu miaka 13 iliyopita.

Gari aina ya Toyota Premio iliopolewa kwenye mto huo ndani yake kukiwa na mwili wa Chemjor.

Kiguta alitenga dakika chache akisoma habari na kumkumbuka Daniel Chemjor.

"Nakumbuka jinsi tulikutana kwa mara ya kwanza Standard Group miaka 13 nyuma..." Alitokwa na chozi huku akionyesha kuguswa zaidi na kifo hiki.

"Hatimaye tukakutana Media Max akiwa katika jopo liliounda kitengo cha Punchline.Nimepata taarifa kuwa alipaswa kuelekeza taarifa hizi za habari na kwa hiyo kila mtu anayefanya kipindi hiki amehuzunika zaidi..." Alisema Kiguta.