Mswada wa punguza mzigo waleta mgawanyiko Nairobi

nrb
nrb
Mswada wa punguza mzigo umeleta mgawanyiko miongoni mwa wajumbe wa Nairobi hata kabla ya umma kushiriki kwenye mswada huo.

Katika kikao chao cha kwanza Jumanne baada ya mapumziko ya mwezi moja, kaimu spika Chege Mwaura alielekeza mswada huo upelekwe kwa wakazi ili watoe maoni yao.

Vile vile alielekeza kwamba kamati ya sheria na masuala ya sheria ichukue jukumu la kushughulikia mswada huo, unaofadhiliwa na chama cha Thirdway Alliance.

Mnamo julai 30,2019 kabla ya wajumbe hao kwenda mapumzikoni, kamati hiyo ilikuwa imejadili juu ya muswda uliopendekezwa na kutatuliwa ya kwamba ilani ya hoja yake ya idhini inapaswa kuletwa na kiongozi wa wengi bungeni.

Spika huyo alielezea gazeti la The Star kuwa anataka njia tofauti humu jjijini Nairobi ambapo mswada huo utapitishwa kwa kuzingatia maoni ya wapiga kura, hatua tofauti na kaunti zingine. Spika huyo alisema zaidi kuwa watagawanya Nairobi katika maeneo angalau nne au tano ili kufanikisha ushiriki wa umma.

Upinzani ukiongozwa na kiongozi wa wachache Elias Otieno walisimama kidete na kusema kwamba wao hawaungi mkono mswada huo. Vile vile wajumbe kadhaa kutoka kambi ya Jubilee wanaunga mkono mswada huo huku wengine wakiamua kutotangaza msimamo wao.