Mtalipa! FKF yaagizwa kumlipa aliyekuwa kocha wa Harambee Stars 108M

amrouche. jpg
amrouche. jpg
Mahakama ya kushughulikia masuala ya spoti imeiagiza FKF kumlipa aliyekua kocha wa Harambee Stars Adel Amrouche Shilingi milioni 108 kama malipo ya kumfuta kazi kimakosa.

Kocha huyo raia wa Ubelgiji alifutwa kazi na aliyekuwa rais wa FKF wakati huo Sam Nyamweya baada ya kupoteza kwa Lesotho katika mechi ya kufuzu kwa AFCON mwaka wa 2015. Aliishtaki FKF kwa FIFA na kuwawadiwa shilingi milioni 60 lakini hakutosheka na kuwasilisha kesi yake kwa mahakama ya spoti.

Rais wa sasa wa FKF Nick Mwendwa alipinga rufaa hiyo lakini akapoteza.

Hayo yakijiri, mshambulizi kinda Gabriel Martinelli alifunga mabao mawili na kuwapa Arsenal ushindi dhidi ya Standard Liege katika ligi ya Uropa.

Kulikua na pengo la chini ya dakika tatu kati ya mabao ya kinda huyo wa miaka 18 raia wa Brazil, huku mwenzake Joe Willock wa miaka 20, akifanya mambi kuwa 3-0 kabla ya muda wa mapumziko. Martinelli, alisajiliwa kwa kititta cha pauni milioni 6 msimu huu joto. Arsenal sasa wako kileleni mwa kundi F.

Kiungo wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang ametumia mtandao wa Twitter kuwasuta wanaosema kua aliondoka Borrusia Dortmund kwa sababu ya pesa tu.

Madai hayo yalitolewa na afisa mkuu wa Dortmund Hans-Joachim katika mahojiano na jarida moja la Ujerumani. Aubameyang mwenye umri wa miaka 30 raia wa Gabon alihamia Arsenal kutoka klabu hio ya Ujerumani kwa kitita cha pauni milioni 56 mwezi Januari mwaka 2018.

Aliyekuwa mshambulizi wa Nigeria Isaac Promise ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 31. Klabu yake ya Marekani Austin Bold inasema alifariki jumatano usiku lakini hawakueleza chanzo cha kifo chake. Promise alikuwa nahodha wa Nigeria waliposhinda nishani ya fedha katika Olimpiki ya mwaka 2008 jijini Beijing. Alitumia muda mwingi wa tajriba yake Uturuki huku pia akicheza Saudi Arabia.