Mtasema Mchoke! Mamake Diamond  Awachoma wakosoaji wake  kwa vijembe mtandaoni.

 Sandra Dangote  mamake msanii wa Tanzania   Diamond Platnumz  amesema  amechoka kumfurahisha kila mtu katika maisha yake na sasa yuataka kuishi kama anavyotaka yeye

Sandra ,amekuwa akipata ukosoaji mkubwa sana kwa ajili ya mtindo wa maisha yake kwa sababu kando na kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mwanamme mwenye umri wa chini  kumliko ,pia mtindo wake wa mavazi haujawapendeza wengi hasa kutokana na imani yake ya dini ya kiislamu Lakini Sandra amesema amefika mwisho na kamwe wanayosema watu hayatamzuia kuishi mtindo wake wa kujiachilia . Amepigisha ujumbe mkali akisema :

‘ISHI UKIAMINI KUA KWENYE HII DUNIA HUWEZI KUMFURAHISHA KILA MMOJA… NA UKITAKA KUFELI KABISA ENDELEA KUJITAHIDI KUWAFURAHISHA WATU WOTE…(LIVE THINKING YOU CAN PLEASE EVERYONE IN THE WORLD, IF YOU WANT TO FAIL CONTINUE TRYING TO PLEASE EVERYONE.’)

  Sandra amekuwa akiwakwaza wengi hasa kwa kupiga picha za  kila mara akiwa na mpenzi wake hadharani tabia ambayo wengi wanasema inafaa kuachiwa rika la mwanawe Diamond na mpenzi wake Tanasha Donna na sio mama wa umri  kama wake . Sandra amesema  watu wanafaa kuyajali maisha yao na wala sio kujishughulisha na juhudi za kuwaangamiza wenzao.  Kama hujapata ujumbe basi hashtag yake ya     inafaa kukupa taswira ya anachosema .