Mtindo wa nywele aina ya 'box' wamsababishia mwanamke kifo

Mwanamke auawa kwa upanga aliotumia katika jaribio la kumuua bintiye Naivasha.

Ijapokuwa stakabadhi za mahakama zilionyesha kuwa  kifo cha Esther Wambui hakikuwa cha maksudi,lakini Gideon Kibunje atasalia gerezani kutumikia kifungo cha miezi 14 kwa kosa la kuua bila kukusudia.

Kibunje ambaye awali alikuwa ameshtakiwa kwa kosa la mauaji, alijitetea kwamba hakuua kwa kukusudia na ombi lake kortini likakubaliwa.

Akijitetea mbele ya Jaji Richard Mwongo kwenye mahakama ya Naivasha, mshukiwa mwenye umri wa miaka 28 alijitetea kwamba alitekeleza mauaji hayo ili kumkinga bintiye.

Aliambia korti kuwa mnamo Januari 14 saa 7 usiku, alifika nyumbani kwake mtaa wa Site mjini Gilgil na Wambui akamwambia alihitaji mboga na maziwa ya jioni.

Kibunje alitoka na kununua bidha hizo muhimu na aliporejea aligundua kuwa mke wake alikuwa amenyoa nywele mtindo wa 'box'. Mtindo huo haukumfurahisha mumewe.

"Nilimwambia kuwa mtindo wa nyewele aliyokuwa amenyoa haufai mwanamke aliyeolewa na hakufurahishwa na maneno hayo,'' alisema.

Kibunje alisema kwamba ugomvi ulizuka na Wambui akakereka zaidi. " Alifungua begi langu na kutoa simi na kumdunga binti wetu. Nilichukua hatua za haraka na kumwepesha mtoto," alisema.

Lakini wakati Kibunje alipokuwa anajaribu kufungua mlango, ili kumhepesha mtoto, Wambui alimdunga na simi mgongoni. Na katika hali ya vuta ni kuvute ili ajiokowe na pia kumuokoa mwanawe, Kibunje alimdunga mkewe kifuani.

Familia hiyo ina watoto wawili wenye umri wa mwaka moja na mitatu.

"Nilikimbia nje na kuomba usaidizi kutoka kwa majirani. Walipofika walimpata akiwa katika kidimbwi cha damu huku amekata roho," alisema.

Hatimaye polisi waliwasili wakamtia mbaroni na kuchukua mwili wa marehemu..

Upasuaji ulifanya na daktari Titus Ngulungu na uchunguzi ulibaini kuwa aliaga dunia kutokana na majereha kwenye mbavu zake kutoka na jeraha la kudungwa kisu.

"Familia yangu imesambaratika na nahitaji kupanga upya maisha yangu na ya familia, hususan watoto wangu ambao hawakuhsika kivyovyote vile katika kisa hicho.