Mto wa vifo!Gavana Mike Sonko azungumza na akina mama

sonko-696x464
sonko-696x464
Timu inyosafisha mto wa Gong katika mtaa wa Embakasi kusini kaunti ya Nairobi Jumapili walipata mili mitatu ya watoto wachanga wakiwa wametupwa eneo hilo.

Hii inaleta jumla ya mili,28, iliotolewa na timu ya Sonko rescue team na kikundi cha Comb green Solution ambacho kinasafisha maeneo hayo.

Baada ya gavana Sonko kutoa kikundi cha kusafisha maeneo ya Nairobi mwaka wa 2018 mili tofauti imekuwa ikipatikana katika mito ya Nairobi huku kisa cha awali kikiwa katika eneo la Korogocho.

Katika mili hiyo ishirini na nane iliopatikana katika mito hiyo 23, ni watoto wachanga na 5 ni watu wazima, alhamisi wiki jana mwili mwingine ulipatikana katika eneo hilo na timu hizo.

Gavana Mike Sonko amewashauri akina mama ambao wana umri mdogo waweze kuuliza usadizi iwapo wanapata taabu na changamoto za kuwalea watoto wao.

Aidha gavana huyo amesema kuwa wanaweza wapeleka wanawe katika nyumba za kuwakuza watoto ili wasichukue maisha ya watoto wasio na hatia yeyote.