Mtoto aaga dunia baada ya kunyongwa na nyama Nambale

 
Biwi la simanzi limetandaa katika kijiji cha Khadoda kaunti ndogo ya Nambalw kaunti ya Busia baada ya mtmto mmoja mwenye umri wa miaka kumi na tano kunyongwa na kipande cha nyama hadi kufa.
Mark Ndubi Obada mwanafuniz wa darasa la tano katika shule ya msingi ya wavulana ya kisoko alipewa nyama na mamake kuichemsha jikoni jana lakini alirudi kwa nyumba yao kubwa akiwa anang'ang'ana kuondoa kipande cha nyama kilichokuwa kimekwama kooni mwake.

Ndug zake Ignitius Mariga mwenye umri wa miaka ishirini na minne na alfred Barasa mwneye umri wa miaka kumi na miwili wanasema walijaribu kuokoa maisha yake kwa kujaribu kukiondoa kipande hicho kooni bila mafanikio huku akizirai na kuaga dunia dakika tano baadaye.