Mtoto Mwaka Moja Aepuka Kwenye Ajali Vihiga (Photos)

Mtoto Adiya Ambani mwenye umri wa mwaka moja na miezi tano ameponea chupu chupu baada ya gari waliomokuwa wakisafiria pamoja na familia yake kuhusika kwenye ajali mbaya. Ajali ilisababisha kifo ya yaya wake  na kuweka wazazi wake kwenye hali mahututi.

Akizungumza katika hospitali ya rufaa ya Vihiga babake malaika huyo Bw. John Ambani ameelezea furaha kumwelekea bintiye japo sikitiko kwake kwani huenda mtoto Adiya kusalia na jamaa zao kwa kadhaa kabla ya kuungana nao.

Visa vya ajali barabarani vimesalia kidonda ndugu katika sekta ya usafiri haswa katika msimu wa likizo licha ya serikali kuzatiti kukabiliana ili kupuunguza ongezeko hilo.

courtesy Rehema Osanya