Mtoto wa miezi 6 ni miongoni mwa watu 25 walioambukizwa virusi vya corona nchini

NA NICKSON TOSI

Akitoa takwimu mpya za maambukizi ya virusi vya corona nchini hiyo jana, katibu msimamizi katika wizara ya afya Dr Mercy Mwangangi alisema miongoni mwa watu 25 waliopatikana na virusi hivyo baada ya kufanyiwa vipimo, mtoto wa miezi 6 alikuwa mmoja wa waathiriwa hao.

Mwangangi alisema kuwa tukio hilo basi linaashiria kuwa virusi hivyo havibagui umri na kuwataka wakenya kuwa ange haswa wakati huu ambapo taifa linaendelea kusajili idadi kubwa .

Kwa mujibu wa takwimu hizo ni kuwa, visa hivyo 25 viliripotiwa katika Kaunti za Nairobi na Mombasa ambapo mitaa ya Nairobi ikiwemo  Kariobangi South ilisajili visa 10, Eastleigh-8, Mathare-1, Kawangware-2, Kahawa West- 1 na Umoja-2.

Katika kaunti ya Mombasa, maeneo yafuatayo ndiyo yaliyosajili visa hivyo kulingana na katibu huyo.

Bombolulu-1, Old Town-8 na  Jomvu-1.

Kufikia sasa Kenya imeasajili visa 490 vya maambukizi huku waliopona wakiwa 173.