Mtoto wangu alipakwa busaa kwa kichwa na kuonjeshwa chang'aa

Massawe Japanni
Massawe Japanni
Katika show uipendayo ya Jambo Massawe ijayo kwako kila siku ya wiki kuanzia mida ya saa nne hadi saa tisa, mijadala bomba huchibuka, wageni huwaacha wengi vinywa wazi na muziki huwatumbuiza waskizaji Kenya nzima.

Juzi, Massawe aliwaomba waskizaji wazungumzie kwa uwazi mila na tamaduni manyumbani mwao ambazo ziliwashtua.

Kulingana na mama mmoja ambaye ameolewa Teso, alishtuka wakati ulipofika wa mwanawe kunyolewa nywele kwani alichokiona hakuwa amekiona wala kukiskia tena.

Alisema kuwa siku ya mtoto kunyolewa kina mama wa kutoka upande wa bwanake, walipika pombe aina ya Busaa na kumpaka mwanawe mwili mzima kabla ya kumnyoa.

Isitoshe, mwanawe alionjeshwa pombe aina ya chang'aa siku tatu baada ya kuzaliwa. Kisa na maana? Eti mtoto aki tabasamu watajua kwa kweli ni mmoja wao.

Soma usimulizi wake na kama huamini skiza kanda ifuatayo ili upate uhondo kamili.

Mimi nilikuwa nimeoleka kule Teso na nikazaa mtoto kijana. Massawe walifanyia mtoto vitu zenye sijawahi ona.

Siku ya kunyoa mtoto, walimpaka mtoto pombe ya aina ya Busaa kwa kichwa ndio wakamnyoa eti ndio wajue kama ni wao.

Unajua vile nilizaa baada ya siku tatu walipea mtoto pombe? Walimpea pombe ndio wahakikishe kama ni wao au sio wao, isitoshe walimpea hadi chang'aa.

Halafu siku ya kunyoa wakatengeneza hiyo Busaa wakampaka mwili wote ndio kina shosho wakamnyoa. Bwanangu kulingana na mila zao ndiye alitoa fedha za kutengeneza hizo vitu.

Nilikuwa tu hapo na singekataa kwani wangesema mtoto sio wao na sikutaka maneno, niliwaachia wakafanya mila zao zote.

Walimlambisha eti akicheka ndio sasa wanajua ni wao.

Skiza kanda ifuatayo.

&feature=youtu.be