Mudavadi amshutumu Ruto kwa kubadilisha makaazi yake kuwa makao ya kampeini

Kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi amemshutumu naibu wa rais Daktari William Samoei Ruto kwa kutumia makaazi yake Karen kuwa makao makuu ya kampeni za anayewania kiti cha ubunge katika eneo bunge la Kibra Macdonald Mariga.
Mudavadi amesema kuwa Muheshimiwa Ruto anafaa kutumia rasilimali za serikali kuhakikisha kwamba wakenya wanafaidika kutokana na ushuru wanaotoa kwa serikali kwa kupata afya nzuri, elimu, miundo mbinu miongoni mwa huduma zingine. Mudavadi alisema haya katika ofisi za ANC hapa jijini Nairobi siku mbili baada ya kurejea humu nchini kutoka Marekani alipokutana na kuzungumza na baadhi ya viongozi wa serikali nchini humo wakiwemo mkurugenzi wa masuala ya Afrika Mashariki naye mkurugenzi wa masuala ya kupambana na ugaidi.

Aidha, Musalia alikiri kuwa anataka kupata miundo dhabiti atakapochukua usukani katika serikali ijayo ila hilo halitowezekana kwa kuwa watu wamekuwa wakiiba na kushinikiza shughuli za kisiasa. Kiongozi huyo amemwonya Ruto kuwa ofisi za serikali zipo kwa ajili ya kutumikia wananchi katika kuimarisha maisha yao na kuwa wakati watu wanaingia au kuja katiaka nyumba au ofisi za serikali unawaambia kwamba nimewapa chakula na kusahau kwamba ni ushuru wao unatumia.
Halikadhalika, Mudavadi amekituhumu chama cha Jubilee na madai ya kuwahonga wananchi wa Kibra kumuunga mkono Mariga katika uchaguzi huo mdogo wa kibra ifikapo Novemba 7, 2019 na rasilimali za serikali hazifai kutumiwa kwa manufaa ya kibinafsi huku wananchi wakikumbwa na baa la njaa na kulipa ushuru wa kiwango cha juu.

"Wakati watu wanasema 'huyo ni hoteli,' huwa wanamaanisha nini? Inamaanisha Jubilee wanamwaga pesa kinyume na sheria za IEBc." Musalia Mudavadi.
-Habari na Naomi Mainye