Mudavadi asimulia jinsi dadake alivyotekwa nyara na mguu wake kukatwa

mUSALIA mudavadi
mUSALIA mudavadi
"Kuna tatizo miguuni mwangu. Sijihisi vyema." Hayo ni maneno kutoka dadake kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi alipopatikana hospitali baada ya kutekwa nyara na kutafutwa kwa siku kadhaa.

Mudavadi anasimulia masaibu yaliyompata dadake  Serah, katika wasifu wake wa Soaring Above the Storm of Passion na kusema kuwa  ghasia za baada  ya uchaguzi mkuu hazikusasa familia yake, licha ya kwamba babake alikuwa mtu maarufu sana katika serikali ya Moi.

Dadake, Serah, jinsi alivyoandika Mudavadi, anasema kuwa alitekwa nyara na mahasimu wa kisiasa wa baba yake na kumkata mguu.

Baba yake alikuwa maarufu sana baada ya kuhudumu kwa kipindi kirefu katika baraza la mawaziri wa Rais Daniel Moi. Alifariki dunia 1989.

Mudavadi alisema kuwa wakati moja, wakati baba yake alipokuwa akishughulikia kesi ya uchaguzi katika mahakama kuu, dada yake aliyekuwa akielekea kusikiza kesi hiyo alifuatwa na kutekwa nyara na baadaye kuachiliwa katika misitu ya Nairobi.

Mudavadi anasema kuwa dada yake alikuwa ameshuka tu kutoka  basi katika eneo la Donholm.

"Walimpeleka msituni, kumkata mguu wake na kumwacha afe," anasema.

"Baada ya kutekwa nyara, tulianza kumsaka kila mahali na tukampata hospitali baadaye."

Ni wakati huo ambapo Serah alimwambi Mudavadi kuwa hakuwa anahisi kuwa na mguu wake tena.

Aidha Musalia anasimulia kuwa dadake hakujua kilichomfanyikia, hakujua kuwa mguu wake ulikuwa umekatwa.

"Waliomteka nyara huenda walikodiwa kutekeleza unyama huo," alisema.

Ijapokuwa Serah alinusurika kifo, aliathirika sana na maisha yake yakabadilika huku madaktari wakisema kuwa hangeishi kwa muda mrefu sana.

Baadaye alipelekwa Israel na hata United Kingdom kwa matibabu zaidi lakini madaktari wakasema kuwa aliathiriwa sana na mguu wake haungepona.

Serah alilazimika kuishi katika hali hiyo hadi kifo chake.