Mudavadi amesema mikutano hiyo inahatarisha maisha ya wakenya hasa katika maeneo ya mashambani ambao wanahudhuria mikutano hiyo .
Wanasiasa wakiwemo maafisa wakuu wa serikali na mawaziri wamekuwa wakifanya mikutano na wananchi huku wakikosa kutii kanuni za wizara ya afya kuhusu kuzuia usmbaaji wa virusi vya corona .
Mudavadi amesema mikuano hiyo inawatia wakenya wengi hatarini.
“ virusi hivi ni hatari na tunafaa kuwa na tahadhari ili kuwalinda watu wetu kwa sababu wengi huenda wakaambukizwa virusi hivi’ amesema Mudavadi .
Mudavadi amesema eneo la magharibi ndilo linalowekwa katika hatari zaidi kwa sababu ya kuzidishwa kwa shughuli za kisiasa . Ameongeza kwamba kanuni za wizara ya afya zimepuuzwa katika mikutano hiyo .
Mawaziri Peter Munya (Kilimo), James Macharia (Uchukuzi ) na Eugene Wamalwa (ugatuzi ) wamezuru eneo hilo ili kuzuru miradi ya maendeleo na kuwa wageni wa magavana wa kaunti za magharibi .Mudavadi amesema wenyeji wengi wamekuwa wakihudhuria mikutano hiyo bila kuzingatia masharti hayo yaliyowekwa .