Waakilishi hao walimhakikishia kwamba wako tayari kumuunga mkono katika nia yake ya kuwa rais ili kumrithi rais Uhuru Kenyatta .
“ Amekuwa wakikutana na viongozi mbali mbali na makundi tofauti kutoka Mlima Kenya katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita na sasa yuko tayari kwenda eneo hilo kujitangaza’ amesema msemaji wake Kibisu Kabatesi.
Mudavadi tayari amekutana na kiongozi wa chama cha Narc Kenya Martha Karua na aliyekuwa mbunge wa Gatanga Peter Kenneth.
Mkutano na wawili hao mwezi mei mwaka huu pia ulihudhuriwa na Slly Kosgey aliyehudumu kama mkuu wa utumishi wa umma chini ya utawala wa rais wa zamani Daniel Moi .
Baada ya kukutana na Mudavadi ,Karua aliashiria uwezekano wa kuunda muungano wa kisiasa kati ya Narc Kenya na ANC kwa uchaguzi mkuu wa 2022 .
Karua amesema anaendelea kuzungumza na Mudavadi na viongozi wengine wenye maono kama yake kutenegeza muungano thabiti wa kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu ujao .
Kabatesi amesema Mudavadi amekuwa akitayarisha safari zake kwenda eneo la Kati wakati ambapo amekuwa akikutana na viongozi kutoka eneo hilo .