Muigizaji Luwi amsherehekea mpenziwe kwa kusimama naye

104432832_876820106146081_4753599739534817558_n
104432832_876820106146081_4753599739534817558_n
Siku kdahaa baada ya kushambuliwa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na kashfa ya ngono, muigizaji wa kipindi cha Maria Brian Ogana almaarufu kama Luwi amemshukuru kichuna wake kwa kusimama naye wakati huo.

Luwi ambaye ni baba na pia muigizaji alimshukuru mpenzi wake kwa kutembea naye wakati huo alipokuwa anapitia magumu.

Amemshukuru kichuna huyo kwa kuendelea kuwa imara katika uhusiano wao licha ya kusoma taarifa potovu zilizokuwa zinamhusu.

Akiandika ujumbe huo, Luwi aliongezea picha ya mpenziwe huyo na ambapo maelfu ya mashabiki wanaomfuatilia walimpongeza kwa kuchukua hatua hiyo.

Wiki moja iliyopita, Jacque Naisenya ambaye ni mpenzi wa Luwi alilazimika kuingilia kati baada ya watu kuita Luwi kama jamaa anayependa wanawake.

Jacque alisema kuwa ataendelea kusimama na mpenziwe wakati wa mazuri na mabaya.

Aliongezea kuwa watu siku hizi wameanza kutumia mitandao ya kijamii vibaya na kuharibia wengine sifa zao.

Luwi alikashifiwa na  mwanamke kwa kutaka  kumlipisha alfu 150 kwa lungula.

Mwanamke huyo alisema kuwa alimwandikia ujumbe Luwi kupitia ukurasa wake wa Instagram akitaka washiriki mchezo usiokuwa na mwamuzi japo na alipotuma pesa hizo, jamaa akatokomea.