Mulamwah amkosoa Ringtone kisa kizungu kombo

2134q
2134q
Fundi na mtaalam wa ucheshi nchini na anayetamba kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii Mulamwah amempiga vijembe staa wa nyimbo za injili Ringtone katika posti yake aliyoichapisha katika mtandao wa kijamii wa insta.

Soma hapa uhondo:

https://www.instagram.com/p/ByuMBrvHDQH/

Katika posti hiyo, Ringtone amepigwa picha na mwenzake Bahati  akimsihi amsaidie katika juhudi zake za mchwa za kumpata bibi atakayemuoa. Ni jana tu Apoko alipofukuzwa katika kanisa la Askofu Allan baada ya kufika na bango lile kanisani humo na kutoroshwa mbio kama mbwa hatari.

"Rudi uchukue school fees yako kwa mwalimu wa English." alimpiga kijembe Ringtone.

Soma hapa hadithi tofauti:

Tatizo la kumpata mke mwema muimbaji huyu limekuwa dondasugu kwake. Katika kipande cha video alichokichapisha katika mtandao wa insta, Ringtone anaonyesha vyombo chafu katika nyumba yake na kuomba wafuasi wake wamsaidie kumpata mwanadada amsaidie kuviosha.

https://www.instagram.com/p/By4yuDGnga9/

Juhudi zake za kumapata mke zinaonekana kuwa zimepiga kasi zaidi mpaka wakati huu ameamua kufika katika mlima wa Ngong ili kumwomba mungu apate mke wa sifa alizoziandika katika bango lake.

https://www.instagram.com/p/BynBFZOn2TJ/

Je, kuna uwezekano hizi ni kiki? Kiki kama hizi katika tasnia ya muziki wa injili ni freshi au sio freshi? Na je kwa kauli yako, unadhani Ringtone kwenda mlima wa Ngong kuomba mke ni utu uzima?