‘Mume wangu aliambukizwa HIV na mbochi, akaniambukiza – sote tuna mimba’

woman
woman
Kuna makubwa yanayoweza kukupata ukashangaa ni vipi utajinasua lakini hakuna cha kutosha kama masaibu anayopitia mwanamke mmoja  ambaye  ameyasimulia mitandaoni

Jane  amekuwa katika ndoa na mume wake kwa miaka 8 sasa na wamebarikiwa kuwa na watoto wawili. Walipopata mtoto wao wa pili, Jane alirejea kazini na ikamlazimu kumtafuta mfanyikazi wa nyumbani ili aweze kumtunza mwanawe naye arejee kazini.  Kwa miaka miwili sasa wamekuwa na mfanyikazi huyo ambaye Jane amesema alikuwa kama malaika.

“Watoto walimpenda na alifanya kazi zote za nyumba bila kuambiwa. Tulikuwa kama madada na hata watu wengi hawakujua kwamba alikuwa mfanyikazi wa nyumbani, wengi walifikiri ni dadangu’ Jane anasema kumhusu  yaya wake

Dunia ilimgeukia wakati ambapo Jane alipoanza kusikia uvumi kutoka kwa majirani kwamba  mume wake alikuwa akishiriki mapenzi na mfanyikazi wao wa nyumbani. Mwanzoni, alipuuza hata fikra kama hiyo na hakujisumbua kumuuliza mume wake au hata yule mfanyikazi wake.  Siku moja, Jane akijitayarisha kwenda kazini, alishuhudia yule mfanyikazi wake akitapika na akamuuliza iwapo alikuwa mgonjwa. Alimuambia alikuwa akiumwa na tumbo na Jane hakushawishika kwa sababu siku ifuatayo pia alimuona akitapika, pale pale akakumbuka zile fununu kwamba mume wake alikuwa akilala na  mfanyikazi wa nyumbani na kwa kweli, alithibitisha kwamba wawili hao walikuwa wakishiriki mapenzi pasipo na Jane kujua. Aligundua kwamba uhusiano wao ulianza kitambo na ilimuuma sana Jane kufahamu kwamba alikuwa akiishi na mke mwenza katika nyumba yake!

Jane hakuweza kufanya kazi siku hiyo na alipokuwa kazini alimpigia mumewe simu kumueleza kwamba anajua kinachofanyika katikati yake na   yaya wao. Mume wa nyumba hakushtuka na alichomuambia Jane kilimshtua.

‘  Aliniambia kwamba ninafaa kuwa na uvumulivu na uelewa kwa sababu ‘mwenzangu’ alikuwa na mimba na hivyo basi nafaa kumpa usaidizi kama alionipa nikiwa na mimba pia.’ Jane anasema

Usaliti huu mara dufu ulimkosesha pumzi na mara akaanguka na kupoteza fahamu. Wenzake walimkimbiza hospitalini  kumbe sasa ndio ngoma ilikuwa imekauka na kipigo kuanza. Akiwa hospitalini, wakimfanyia vipimo , kujua tatizo ni gani waligundua kwamba Jane pia alikuwa na mimba ya mwezi mmoja hivi.  Isitoshe, walipoanza kumpa utunzi wa mama mja mzito walimpima ukimwi na kugundua kwamba alikuwa na  virusi vya HIV ! Jane hakuweza kustahimili habari hizo kwa wakati mmoja. Usaliti wa mumewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi , kupatikana kuwa na mimba bila kutarajia, kugundua kwamba  mfanyikazi wake pia alikuwa na mimba na kugundua kwamba alikuwa kaambukizwa virusi vya HIV  vyote kwa wakati mmoja!

Hakuweza kupata ujasiri wa kutaka kuondoka hospitalini, Jane alimwita mamake kuja kumchukua na pia aende kwake kumletea watoto wake.  Uchungu wa kuambukizwa ukimwi na mumewe aliyeambukiza na mfanyikazi wao wa nyumbani ulikuwa mkali sana na ulimchoma moyo hadi sasa .

Ungefanya nini iwapo ungejipata katika hali ya Jane?