Mume wangu anataka watoto ila hataki nipate periods - Ruth

Kama kuna shabiki ambaye amewahi mshtua mtagazaji Massawe Japanni ni mwanadada kwa jina Ruth ambaye alifichua masaibu aliyopitia katika uhusiano wake.

Kulingana na Ruth alikuwa kwa uhusiano na jamaa ambaye hakuwa anafahamu lolote kuhusu hedhi na hakuwa anaelewa kuwa mwanamke akiwa na hedhi hapaswi kushiriki ngono.

Ruth alisema kuwa mpenziwe licha ya kuwa na miaka 25 alikuwa anasisitiza wawili hao washiriki mapenzi na kila anapokataa, alikuwa anampiga na kumskuma.

Hilo lilimfanya atoke na kutorokea kwao nyumbani.

Hata hivyo ilibainika kuwa aliyekuwa mpenziwe Ruth alisoma hadi darasa la nane.

Soma usimulizi wake,

Mwanamume mwenye umri wa miaka 25, hakuwa anataka kuskia mambo ya kupata periods na ukimwambia una periods anasema unadanganya, anakuchapa anakusukuma anasema ati anataka haki yake na mimi nikipata periods huhisi tumbo inaniuma.

Yaani alilulizwa na brother yake akasema hajui wanawake huwa na periods na nilivumilia kwa hiyo ndoa kwa miaka kumi na alikuw amefikisha masomo hadi darasa la naye.

Aki alinichokesha na nikatoka nikaenda kuishi na wazazi wangu aki nikiskia amekufa naweza rudi mbio kwao ili nikatulie na watoto wangu juu nimechoka.