'Mume wangu wa zamani alikodi wahuni kuniua,’ Mwanamke asimulia

Hanifa-compressed
Hanifa-compressed
Miezi mitatu baada ya kumpa talaka, mumewe Hanifa alimrai atembelee wanao wawili.

Kwa kweli jambo usilolijua ni kama usiku wa giza, na Hanifa hakujua kwamba huu ulikuwa mtego maalum uliopangwa na mumewe kulipiza kisasi. Na hadi leo anakumbuka kusimulia kwa uchungu masaibu yaliyompata alipoitikia wito huo.

Hanifa Nakiriowa ameachwa na makovu usoni na jicho lake la kulia kupoteza uwezo wa kuona baada ya aliyekuwa mume wake kukodi wahuni kumshambulia kwa asidi kali aina ya Sulphuric wakati alipotoroka ndoa ya mateso.

Ilichukua Nakiriowa zaidi ya miaka mitano  na upasuaji 28 ili midomo yake ya juu na ya chini kufungana na kurudi katika hali ya kawaida. Ijapokuwa, alipona aliachwa na makovu yatakayodumu milele.

Uso unaong’aa, ngozi ya rangi ya chokoleti, na macho ya kutabasamu na kope zinazoelea. Kwa hakika sura ya Hanifa ilikuwa yenye kuvutia na pendeza.

Kila aliyemwona alikirii kuwa ni mrembo kupindukia. Hiyo ilikuwa ni taswira yake kabla ya ua hilo la waridi kugeuka na kuwa kovu kubwa linaoshiria kunusurika kifo.

Hanifa, mwenye umri wa miaka 37, alinusurika kifo mnamo Desemba 2011. Na miaka 8 baadaye anashukuru Mungu kuwa hai kusimulia masaibu yake.

Mnamo 2003, wakati akisomea digrii yake katika chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda, Hanifa anakiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mhadhiri wake wakati huo.

Mwanzoni, mapenzi yake yalielea kabla ya kunata na wawili hao kuzama katika bahari nzima ya mapenzi isiyo na kifani.

Wanasema, mwanamke akipenda kwa moyo wake wote, huwa amependa kweli. Na Hanifa alionekana kubebwa katika upeo huo wa mapenzi uliovuma kwa kasi asjitambue.

Walikaa pamoja na Kufikia wakati wa kuhitimu kwake chuoni 2006, walikuwa wanatarajia mtoto wao wa kwanza.

Hanifa anakiri kwamba baada ya kitinda mimba wao kuzaliwa, mapenzi yao yaligeuka na ua la mapenzi yao likanyauka.

"Baada ya kujifungua, nilipokea ujumbe wa pongezi kutoka kwa rafiki wa kiume na hapo ndipo mkondo wa mapenzi yangu yalianza kubadilika," Hanifa aliambia Radio Jambo.

Uhusiano wake na Mumewe

Mumewewe ambaye jina lake tumelibana, hakufurahishwa na ujumbe aliotumiwa Hanifa.

Alianza kumzuia Hanifa kufanya kazi au kusoma tangu siku hiyo.

Alitaka Hanifa awe mama wa kukaa nyumbani na kuwalea wanao wawili.

‘Sikuweza kustahimili amri hiyo. Nilikuwa na ndoto za kutimiza katika maisha yangu, nilikuwa na elimu na nilitaka kuwa huru," alisema

Hata hivyo mumewe akazidi kudhibiti na kumyanyasa zaidi. Hanifa aliamua kumtaliki mumewe mnamo Oktoba 2011, baada ya miaka saba ya ndoa.

"Nilikimbia ndoa. Nilimpa talaka kwani yeye alikuwa ananinyanyasa sana. Hakutaka nisome au nifanye kazi au kuwa na maoni yanayopingana na yake," anakumbuka.

Walikuwa na watoto wawili wakati huo, Hanifa aliwaacha chini ya ulezi wa baba yao na akatorokea kwa kaka yake nyumbani Kampala.

Kushambuliwa kwa Asidi ya Sulphuric Usoni

Miezi mitatu baada ya kumpa talaka, mumewe ambaye alikuwa ameachana naye  alimuita atembelee watoto wao.

Kwa kweli jambo usilolijua ni kama usiku wa giza, na Hanifa hakujua kwamba huu ulikuwa mtego maalum ya mumewe kulipiza kisasi.

“Nilikwenda nyumbani kwa mume wangu wa zamani kutembelea watoto wangu. Sikuwa nimewaona kwa miezi mitatu.”

Aligonga mlango. Kwa ndani, alisikia mchakacho wa nyayo, lakini hakuna mtu aliyejibu. Kisha kijana ambaye hakujua alitokea na akamwagia likwidi usoni.

"Mara nikahisi baridi usoni mwangu. Lakini katika sekunde chache, nilihisi uchungu sana, nilidhani nilikuwa nimetupwa katika dimbwi la moto.” Hanifa anakumbuka.

"Unaungua moto usioonekana.’’

Majirani walimsihi mumewe ampeleke Hanifa hospitalini.

"Mwishowe alifungua mlango, alisema hangeweza kupata ufunguo wa gari lake", alisema Hanifa.

Jirani akamkimbiza hospitali ya karibu ambapo alipewa huduma ya kwanza na kwa bahati nzuri alinusurika kifo.

Mwanzoni, Hanifa hakuelewa kiwango cha majeraha yake lakini alipoangalia kwenye kioo hakujizuia kulia.

Nusu ya mdomo wake ulikuwa umechomwa na makali ya asidi, misuli kwenye midomo yake ilikuwa na imeachana na kuacha pengo wazi amablo Hanifa hangeweza kutabasamu.

“Sehemu za pua yangu ilikuwa imechomeka vibaya sana, pua yangu ilikuwa ikamefungana sikuweza kupumua.

Nilipoteza jicho moja. Uso wangu wote ulikuwa umeharibika. Hiyo ni mara ya kwanza nilivunjika moyo na kulia, "alisema.

"Familia yangu ilijaribu kunituliza, na niliwaambia waniache, ninahitaji muda wa kulia. Nililia kwa muda mrefu."

Madaktari walisema ilikuwa shambulio la asidi aiana ya sulphuric.

Alifikisha kesi Mahakamani akimtuhumu mumwe wake kwa kupanga na kufahdili shambulizi hilo la kulipiza kisasi dhidi ya kumtaliki mumwewe na kutoroka kwake.

Hata hivyo, anasema kuwa mumewe aliachiliwa kwa dhamana na mahaakama.

Hanifa aliondoa kesi yake mahakami baada ya kuona kwamba hangepata haki.

Aliondoka hospitalini baada ya miezi kadhaa ya upasuaji upya na akajifunika kwa kitambaa kwa kuhofia unyanyapaa.

"Kila wakati nilijaribu kujificha kwa kujifunika na kitamba katika uso wangu nilikuwa najaribu kujificha. Upweke ukanipata, sio amani. Lakini nilijimotisha kuwa ni lazima nikubali jinsi hali yangu ilivyo na pia kuipa nafasi na umma unikubali. Huyu ni mimi. Ilibidi nifunue uso wangu," alisema.

Anajipa moyo kwa kukinai na kukubaki hali ilivyo., "Nitafanya haya makovu kuwa alama za nyota katika maisha yangu. Kilio hakitanisaidia. Ninahitaji kufikiria hatua yangu inayofuata na nimekubali kuwa nitakuwa hivi katika maisha yangu yote."

Ilichukua zaidi ya miaka mitano na upasuaji 28 wa kurekebisha upya hali ya midomo yake na kuzuia maumivu. Huwa nadra sana kwake kutabasamu.

Mwanaharakati

Hivi sasa yeye ni mtetezi wa waathiriwa wa ‘shambulio la asidi’ na aliunda shirika la CERESAV ili kuwapa ushauri nasaha na kuwsaidia wanaonusurika katika majanga hayo kukubalika katika jamii.

Mbali na kazi zake za nyumbani na harakati za utetezi, yeye anapenda sana kujumuika na familia yake.

Uso wake huuonekana kuwa anagavu na yenye matumaini kila wakati anapozungumza  juu ya binti zake wawili ambao wana bidi ya kujifunza na kuelimika.

"Nimepata fahari kwa kusoma vitabu vya kunimotisha,” anasema.