‘ Mume wangu wa zamani alizaa watoto 9 na wanawake tofauti kabla ya kifo chake’

woman crying.
woman crying.
Mjadala kuhusu mbona wanaume wa Kenya huwa hawawatambui wanao hukithiri kila mara mtu mashuhuri anapoaga na kisha msururu wa wanawake kujitokeza kudai kwamba ni baba ya watoto wake .

Je ni vyema kuficha watoto uliozaa nje ya ndoa? Mwanamke mmoja amesimulia jinsi marehemu mume wake alivyozaa watoto 9 na wanawake nje ya ndoa kabla hajafa.

 Nilikutana  naye baada ya shule ya upili  na kuanza kupata watoto. Watoto wangu sasa wana umri wa kati ya miaka 16 na 19  hata hivyo hatukufunga ndoa  naye akapata watoto wengine watano  na wanawake tofauti

Anaongeza

 Nawajua watoto wote na huwa anawatunza. Hata najua mwanamke  ambaye anaishi naye  na kati ya wanawake wote aliopata watoto nao. Ni mimi pekee ambaye nimempa mtoto msichana. Ndio kwa sababu hawezi kuniacha

 

Anaongeza

 Niligundua kwamba alikuwa na mke na watoto wakati nilipopata mimba yake. Kinachoshangaza ni kwamba, alinifanya nihisi kwamba nilikuwa mwanamke pekee katika maisha yake, baadaye niligundua alikuwa na watoto wengine tisa

 Nilipoitwa na kuambiwa kwamba ameaga dunia, niliamua kusalia kimya kwa sababu sikutaka drama

Kwa kutamatisha anashauri hivi

 kama mwanamke, ni uamuzi wako kujua utakavyochukulia habari za kugundua kwamba  mko wengi katika maisha ya mwanamme .