Mumewe Janet Mbugua awapa ushauri wakenya

janet.mbugua.and.eddie.ndichu(1)
janet.mbugua.and.eddie.ndichu(1)

Baada ya ndoa yake na mpenziwe Janet Mbugua kuvunjika, mumuwe Janet amewapa wakenya ushauri kwa kuwambia wawe na mawazo ya kuwajenga kibinadamu licha ya hali wanazapotitia.

Ndichu, ambaye bibiye,Janet Mbugua , aliacha kumfuatilia katika mitandao yake ya kijamii aliandka,

"Kuchagua kuishi ukiwaza vyema licha ya hali ngumu inanisaidia kujipa furaha machoni mwangu. Fanya uwezalo leo kisha ya kesho mwachie mwenyezi Mungu yote."

Mmoja wa wafuasi wake alisisitiza maneno yake kwa kusema,"Kweli kabisa. Nimepata ushauri sasa hasa wakati huu ambapo nipo safarini ya siku 30 mwezi huu."

Mnamo siku ya kusherehekea wamama wote duniani, Ndichu aliweka picha ya mamake mzazi kisha kuijaza na maneno ya kumshukuru.

Hakuweka picha ya bibiye kumtakia siku ya kina mama yenye fanaka na furaha kama alivyozoea miaka ya hapo mbeleni.

Siku ya kusherehekea kina baba, aliyekuwa bibiye hakumsherehekea Ndichu wala kutaja lolote linalohusiana na penzi lao.