'Mungu anachukia talaka,'Alikiba azungumzia madai ya kutengana na mkewe

Uvumi umekuwa ukienea kwa muda sasa ya kwamba msanii wa bongo Alikiba wametengana na mkewe Amina Khalef huku hakikosa kuzungumzia suala hilo na kukimya hatimaye msanii huyo amezungumzia suala hilo huku akisema kuwa hajawahi tengana na mkewe.

Akiwa kwenye mahojiano na Cloud FM alisema kuwa alijaribu kusema kuwa wako sawa na kewe endapo swali hilo lingeulizwa kwenye mahojiano yeyote laki i hamna yeyote ambaye alimuamini.

"Alikuwepo siku zote, mbona mnafikiria hivyo ama kwa sababu mmeona picha. Tuko vile vile freshi siku zote nilikuwa nawaambia lakini mlikuwa hamuamini." Alisema Kiba.

Awali akiwa kwenye mahojiana msanii huyo alidai kuwa walikuwa na matatizo fulani lakini hawajatengana, maneno yake msanii huyo yanajiri miezi chahce baada ya habari kutoka Tanazania kudai kuwa wawili hao hawayuko pamoja.

Alikiba aliwaonya wanamitando dhidi ya kusherehekea matatizo ya wenzao, kwa maana mwishowe watayafanya mambo yawe mabaya zaidi.

"Ni kweli mimi na mke wangu tuna migogoro na ni jambo la kawaida kwenye ndoa, ila sijampa talaka hata moja”...“Watu wasipende kufurahia matatizo ya wenzao, au labda ni ukosefu wa kazi, hakuna jambo ambalo Mwenyezi amelihalalisha na analichukia kama talaka. Binadamu unapata wapi ujasiri wa kuchochea wenzako waachane kwenye ndoa, ni shetani tu ndio anapenda ujinga huo."