Mungu hajanichukia kwa kumpa Kanyari talaka-Betty Bayo

Z
Z
Wanawake wengi hupitia masaibu mengi katika ndoa na kuteseka huku wakivumilia kwa hofu kuhusu vile jamii au rafiki watasema endapo wataondoka kutoka ndoa hizo.

Ni hali ambayo mwanamziki wa injili Betty Bayo aliyeteka nyoyo za wengi kwa miziki yake mitamu alipitia akiwa mke wa mhubiri mwenye utata Kanyari.

Anawashauri wanawake ambao wanadhulumiwa katika ndoa wasiweze kukaa katika ndoa kama hizo kwa maana ni wao watakaoumia.

Aliandika katika mtandao wa Youtube na kuwashauri watu wasiweze kukaa katika ndoa za dhuluma.

"Mungu anachukia talaka lakini hachukii wanatalaka, kwa maana anaelewa shida na mateso ambayo wanapitia katika ndoa za dhuluma," Betty Aliandika katika mtandao wake wa Youtube.

Mwanamziki huyo alijulikana sana kwa wimbo wake wa "Eleventh Hour" na kisha kuoana na Kanyari aliyemlimbikizia sifa kede kede na kumtaja kama mwanamume mzuri na mwenye roho nzuri katika sherehe ya kisiri 2012.

Baada ya miaka mitatu wapenzi hao waliweza kutalikiana na kila mmoja kuenda kwa njia yake, Betty alisema alikuwa anataka ndoa ambayo ingedumu na kupata familia lakini hayo yote hayakuweza kutendeka.

"Kama mtu mashuhuri, mashabiki wako wanatarajia mengi  kutoka kwako na hakuna mtu yeyote angetaka unyonge  wake kuonekana na kujulikana hadharani," Alisema Betty.

Betty alisisitiza kuwa hakuna mtu yeyote anafaa kuvumilia ndoa yenye vurugu na kujipata katika msongo wa mawazo na huzuni.

"Nilijaribu sana niwezavyo kuokoa ndoa yangu, lakini ilifikia kiwango ambacho hisia zangu zilididimia kutokana na yale nilikuwa napitia," Alieleza Betty.

Mwanamziki huyo aliweza kuendelea na maisha yake na yuko tayari kufanya harusi kupitia mtandao wake alisema kwamba amechumbiwa.

"Nishaa poa na kuendelea na maisha lakini wakati mwafaka utakapo fika nitaweza kuzungumza, nitaweza kuwaonyesha na kuzungumzia mchumba wangu na hata kuwakaribisha katika harusi yangu,

"Mtamjua nyinyi nyote," Alisema Betty Bayo.