Mungu halali! Muimbaji Kambua ajaliwa mtoto wa kiume

Msanii wa nyimbo za injili na pia mtangazaji, Kambua alibarikiwa na mtoto baada ya kuweza kuificha mimba yake kwa siku nyingi.

Hata hivyo, aliweza kutangaza uwepo wake mungu na baraka ikiwemo tarehe 17 Mei huku akichapisha picha tu mtandaoni bila kuandika chochote.

Baada ya kusumbuka kwa mda mrefu akijaribu kupata mtoto bila mafanikio, Kambua amekuwa akionesha tumbo lake huku uso wake ukibadilika na kungáa zaidi.

Kwa picha zake amekuwa akingáa kama ushuhuda kuwa mungu aweza fanya kuliko makadirio ya wanadamu.

Huku mtangazaji huyo wa runinga ya Citizen akichukua breki kidogo ya wiki kadhaa, tulijua kuwa alikuwa akijitayarisha kujifungua.

Hii leo, rafikiye na msanii Holy Dave, alitangaza katika kipindi cha Bambika kuwa Kambua alijifungua mtoto wa kiume kwa jina, Nathaniel Muhoro Mathu mnamo tarehe 10 Agosti.

Tunamtakia Kambua na mumewe kila la heri katika safari yao ya uzazi huku tukimsheherekea na kumuombea mema maishani.