Mungu mponye!Seneta Priscilla Zawadi alazwa hospitalini baada ya kuhusika katika ajali

machakos-level5-hosital
machakos-level5-hosital
Seneta mteuliwa Priscilla Zawadi Kitsao amelazwa katika hospitali ya Machakos level 5 baada ya kuhusika katika ajali ya barabara kuu ya Malili.

Kamanda wa kaunti ya Makueni Joseph ole Naipeiyan alisema kuwa gari la seneta Priscilla liligongana ana ka ana na gari lililokuwa linaelekea Mombasa saa kumi na moja jioni siku ya Jumatano.

Wahudumu wa hospitali hiyo walisema yuko katika hali njema, wiki iliyopita gari lililokuwa limembeba kiongozi wa wanawake wa Taita Taveta lilimgonga mtu na kumuua papo kwa hapo eneo la Emali wakati wa kafyu.

Kutoka kwetu wanajambo tunamtakia afueni ya haraka.

Mengi yafuata.