'Mungu ndiye sponsor wangu,’ Tanasha Donna azungumzia uhusiano wake na Realtor Mwenda

Tanasha-Donna-and-menda
Tanasha-Donna-and-menda
Wikendi iliyopita Tanasha Donna na Mwenda  Thuranira walitamba sana katika mitandao ya kijamii baada ya uvumi kuenea kuwa wameanza kuchumbiana.

Uvumi huo ulienea baada ya Tanasha kuposti picha yake na Mwenda wakiwa pamoja baada ya kukubaliana bei ya nyumba.

Wengi walibaki midomo wazi  wakisema Tanasha hawezi kuwa na uwezo wa kununua jumba la zaidi ya millioni tano.

Hii ni kwa sababu hajaenea sana kimuziki.

Wengi walisema kuwa ameangukia sponsor baada ya kumuacha staa wa bongo Diamond, kupitia mtandao wake wa kijamii alikuwa na haya ya kusema,

"AIN’T IT SAD HOW A WOMAN CAN’T ACCOMPLISH SOMETHING ON HER OWN WITH HARD WORK, DEDICATION, BRAND POSITIONING WITH THE HELP OF A GOOD TEAM WITHOUT THE MEDIA ASSOCIATING YOUR SUCCESS WITH OTHER MEN.

“WOMAN BUYS A CAR OR A HOUSE OR OPENS BUSINESS PUBLIC PERCEPTION ‘OH MUST BE DATING SPONSOR/RICH GUY." Tanasha Aliandika.

Akiongeza na kunakili,

"WHY CAN’T IT BE ‘SHE MUST HAVE LANDED HERSELF A GOOD DEAL THAT GOT HER A BAG?’. WE LIVE IN THE 21ST CENTURY! DOES SEXISM STILL EXIST? SAD WORLD." Aliandika.

Alifichua kuwa hana sponsor wala mwanaume yeyote ambaye anamsaidia maishani mwake.

“God is my sponsor.” Tanasha Aliandika.

Tanasha aliondoka Tanzania baada ya kutengana na Diamond wakiwa na mtoto mmoja wa kiume.