Chris Kirubi aonekana kuimarika kiafya,mwili wake wanawiri

Bwenyenye Chris Kirubi kutoka Kenya ameonekana akiwa mwenye buheri wa afya kulingana na picha zilizopigwa hivi majuzi mjini i Nairobi.

Kirubi amekuwa wazi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ugonjwa wa saratani, anaopambana nao.

Watu husema kuwa, maisha si ya kuishi kama unasubiri mawimbi yapite bali maisha ni kugundua jinsi ya kuishi huku ukiwa na matatizo hayo na ukijaribu kuzisuluhisha.

Hivyo basi kwa Chris Kirubi ni wazi kuwa ametambua wazi jinsi ya kuishi na ugonjwa huu kwani anaonekana kuwa mwenye furaha tele na mwenye afya si kidogo.

Tazama picha za sasa za Kirubi.