‘Mungu Nipokee’ Soma ujumbe wa Akothee kwa Mola

Sarakasi na  ucheshi wa Akothe hautwahi kuisha  hivi karibuni na sasa ameamua kuanza kutengeza njia ya kwenda Mbungini mapema kwa kumuomba mola msamaha mapema kwa ‘dhambi’ zake .

Jumapili msanii huyo aliwachekesha wengi mtandaoni kwa  sala yake kwa mola akiandika ;

 “Lord ! on this Sabbath day, if it’s my twerking and arrogance that has made you Angry or some other sins that I might have assumed, please find a place in your Kingdom to receive me, just as I am your Child. Please Lord delete their memories so they stop reminding me whatever I did in 1900, and walk me through the New pathway   AMEN  ” 

Posti yake ilipokelewa vyema na mashabiki wake huku wengi wakipata tabasmu kutoka kwayo licha ya changamoto ya sasa ya kupambana na janga la virusi vya Corona .

Wiki jana  yeye na Eric Omondi  walifanya utani kuhusu kupata mtoto pamoja . lakini Akothe akasema ni mapena sana kwa wao wawili kupata mtoto .