Murkomen auliza maswali mazito kuhusu barua ya njama ya Ruto "kuuawa"

qiPJWXQt_400x400
qiPJWXQt_400x400
Baada ya Dennis Itumbi kukamatwa katikati mwa jiji la Nairobi kuhusiana na barua bandia iliodai kuwepo kwa njama ya kumuua Naibu Rais William Ruto, mwandani wa naibu wa rais Murkomen ametokea kukashifu kutiwa nguvuni kwa Dennis.

Murkomen amechapisha ujumbe katika mtandao wa Twitter na kuuliza maswali kibao kuhusu kukamatwa kwa Dennis pamoja na swala nzima la madai ya mauaji yanavyoendeshwa.

Soma hapa hadithi nyingine:

https://twitter.com/kipmurkomen/status/1146373452854697984

"Arrest of  is a strategy to divert attention from the La Mada meeting&plan.Was there a meeting?Did PS in charge of DCI say Ruto must be stopped Saitoti way?Who complained about assassination?And to who?The authenticity of the allegations is more important than a letter."

Kulingana na mwanasiasa huyu, tukio la kumkamata Dennis ni njama ya kufunika na kuyeyusha swala nzima la kufanya uchunguzi wa mkutano uliofanyika hoteli ya La Mada. Murkomen zaidi ya hapo anataka kujua iwapo kuna katibu wa idara ya upelelezi aliyesema kuwa watasimamisha Ruto kama ki-saitoti.

Itumbi ni katibu wa dijitali, ubunifu na mawasiliano ya kimataifa katika afisi ya Naibu Rais. Itumbi siku ya Jumatatu alikashifu gazeti la Daily Nation kwa kuchapisha taarifa iliyomhusisha na barua hiyo.

Soma hapa:

Gazeti hilo lilikuwa na taarifa siku ya Jumapili kwamba wasaidizi wawili wa Naibu Rais William Ruto walikuwa wanasakwa na makachero kwa tuhuma za kusambaza barua hiyo. Taarifa hiyo ilisema wawili hao walikuwa kutoka kitengo cha mawasiliano cha Naibu rais.

Maafisa wa upelelezi wanaochunguza barua inayodaiwa kuandikwa na waziri mmoja wamekuwa wakifuatilia uwezekano kuwa huenda barua hiyo ni gushi.