Murkomen na Raila Junior warushiana cheche za maneno kwenye Twitter

Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen na mwanawe kinara wa ODM Raila Odinga Jumatano, Juni 24 walirushiana makonde kwenye  mitandao ya kijamii ya twitter.

Wawili hao walijibizana kuhusu ujumbe aliokuwa ameuchapisha Murkomen 2017 wakati Raila alikuwa akiapishwa kama rais wa wananchi.

Junior alizungumza kuhusu masaibu anayopitia Murkomen baada ya kutimuliwa na Jubilee kutoka wadhifa wake.

Kijana huyo wa Raila alimkumbusha seneta huyo aliyokuwa ameambiwa hapo awali alipokuwa akimcheka Baba na masaibu yake.

"Kuwa mamlakani ni utamu. Maneno haya yamekuja kumpata Murkomen."Aliandika Raila Junior.

Hata hivyo, Murkomen alikerwa na maneno hayo na kumtaka Raila Junior kumwandikia babake hayo au Ikulu. Alijigamba kuwa ameweza kuafikia makubwa kuliko aliyokuwa ameafikia Raila katika umri alio nao seneta huyo.

Ni majibizano ambayo yalizua hisia mseto kutoka kwa Wakenya wengine kwenye mtandao.

https://twitter.com/Railajunior/status/1275311101236916225