Museveni aamrisha idadi ya madereva waliopatikana na corona kuondolewa katika takwimu kamili za serikali

Taifa la Uganda limeamua kufanyia marekebisho takwimu zake za kitaifa kuhusiana na virusi vya Corona kwa kuondoa idadi ya madereva waliopatikana na virusi hivyo katika sajili yao.

Kulingana na takwimu zilizorekodiwa Jumatano, Uganda ilisajili visa 10 vipya vilivyotokana na madereva  huku wizara ya afya katika taifa hilo ikisema Museveni aliamrisha kufanyiwa kwa mabadiliko hayo.

“Today, 20 May 2020, 10 new COVID-19 cases confirmed. 9 new cases are truck drivers while 1 case is a contact case. Following a Presidential Directive of deducting all foreign truck drivers from Uganda’s total confirmed case count, the confirmed COVID-19 cases now stand at 145,”  wizara ya afya imesema .

Kufikia Jumatano, Uganda ilikuwa imewarudisha madereva 124 katika mataifa yao baada ya kupatikana na virusi hivyo .

Kufikia sasa, Uganda haijasajili kisa chochote cha kifo na inaafikia kupunguza masharti ya kufungua shughuli zote za kitaifa baada ya kusitishwa.

Baadhi ya mapendekezo ambayo Uganda inapania kuchukua ni kufungua shule huku watakaokuwa wa kwanza kurejea shuleni wakiwa watahiniwa wa mwaka huu.