Mutahi Kagwe asema watu 11 wamepatikana na virusi vya Corona

NA NICKSON TOSI

Watu 11 nchini wamepatikana na virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo na kufikisha idadi ya wale walioathirika nchini kufikia wati 281.

Watu wengine 2 wameruhusiwa kuondoka hospitalini hii leo baada ya kupona na kufukisha idadi ya wale waliopona kuwa watu 69, miongoni mwa wawili hao ni daktari.

Jamaa walisafiri hadi Homabay kutoka Nairobi wakiwa na jeneza kwa maazishi feki,Dereva apatikana na Coronavirus

Kati ya watu 11 waliopatikana na virusi hivyo leo, Mutahi amesema 7 wanatoka Mombasa na 4 wanatoka kaunti ya Nairobi eneo la Ruaka.

Watu hao 6 ni wanaume na 5 ni wanawake wa miaka kati 11-80.

Wakati uo huo, Mutahi amesema kufikia sasa serikali imebakisha vituo vya karantini nchini 33 ambavyo vinafanya kazi kwa sasa baada ya kufunga maeneo mengine.

Hatujamalizana na Corona, Mafuriko tena! Watu 4000 wapoteza makaazi yao Bonde la Ufa kutokana na mvua kubwa

Watu 455 wamewekwa chini ya karantini ya lazima baaada ya kupatikana nje mida ya saa 7 jioni kwa kile  Mutahi amesema ni kuhakikisha kuwa kila mtua anafuata maagizo ya serikali.

Aidha Mutahi amesema kuwa wamefanyia mafunzo maafisa wa polisi takriban 1,000 jinsi ya kukabiliana na waathiriwa wa corona.

Wazira ameongeza kuwa wamesambaza vifaa vya kuwalinda maafisa wa afya almaarufu kama PPEs zaidi ya 4,759 katika baadhi ya hospitali ambazo zinatumika .

Kagwe ameongeza kuwa maafisa wa afya zaidi ya 30,000 wanaendelea kupewa mafunzo kote nchini dhidi ya kukabiliana na wagonjwa wa corona.

Visa vya maambukizi ambavyo vimeripotiwa kwa sasa vimetokea katika maeneo ya  kitengele, Kumulu, tana River na  ongata rongai