Muuguzi mkenya aaga dunia siku chache baada ya kupona covid-19

Maelezo ya kina yameibuka kuhusu muuguzi wa kaunti ya Homa Bay aliyeaga dunia siku chache baada ya kupona virusi vya corona,Muuguzi huyo alipatikana na virusi hivyo mnamo tarehe 20, Julai huku baada ya kupimwa vipimo hivyo mara mbili na kuambiwa kuwa hana virusi hivyo mnamo tarehe 29 julai.

Mariam Awuor alikuwa anapokea matibabu katika Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Kisii alimokuwa anapigania maisha yake.

Kulingana na Chama cha Wauguzi Nchini, hali ya marehemu ilidorora siku ya Jumapili, Agosti 2, na kupumua pumzi yake ya mwisho mwendo wa saa kumi jioni baada ya kulemewa na ugonjwa huo.

Akiwa kwenye chumba cha ICU, Mariam alijifungua mwanawe, huku akiwalaumu madaktari wa ICU kwa uzembe wao baada ya kugundua ana virusi vya corona.

Kulingana na Chama cha Wauguzi Nchini, hali ya marehemu ilidorora siku ya Jumapili, Agosti 2, na kupumua pumzi yake ya mwisho mwendo wa saa kumi jioni baada ya kulemewa na hali yake.

"Mariam alijifungua mtoto wa kiume akipokea matibabu.Aliendelea kupokea matibabu ya wagonjwa mahututi ikiwemo kuongezewa oksijeni."

Kulingana na mtendaji wa afya Sarah Omache wa kaunti ya Kisii alifutilia mbali habari kuwa Mariam alitengwa na madaktari bada ya kupatikana na virusi hivyo.

"Tuliweza kuwafuatilia waliokuwa na wao na kuwapeleka karantini, jamaa zake na madaktari waliokuwa wanamtibu ni miongoni mwa watu waliowekwa karantini

Mada kuwa alitengwa baada ya kupatikana na virusi vya corona no uongo." Alizungumza Sarah.

Awuor alikuwa anahudumu katika Hospitali ya Kauntu Ndogo ya Rachuonyo na alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Kaunti ya Homa Bay baada ya kuonyesha dalili za homa lakini hakupatwa na virusi vya COVID-19.

Hata hivyo, alikumbana na matatizo ya kupumua na kuhamishwa hadi katika Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Kisii ambapo alipimwa upya COVID-19 na kupatwa na virusi hivyo.

Swali kuu ni je nini hasa kilijiri baada ya madai hayo kutupiliwa mbali?Ni jukumu langu na lako tuwe salama na kisha kufuata kanuni za wizara ya afya.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.