‘Muulize analala na nani.’ Baby mama wa Ravanny asema akiwa kwenye mahojiano

Fahima almaarufu Fayvanny ni 'baby mama' wa msanii Rayvanny ambaye hivi majuzi walitengana na kuthibitisha kuwa habari hizo ni za ukweli kuwa wametangana. Wawili hao wamebarikiwa na mtoto mmoja.

Mambo yanaonekana bado hayajasuluhishwa kati ya hao wawili. Akiwa katika mahojiano, Fahima hakuwacha mambo yaende rahisi bali alisema kuwa hawaishi kama awali.

Akiwa kwenye mahojiano na Wasafi media aliulizwa huwa analala na nani kando yake na alikuwa na haya ya kujibu.

"MIMI NALALA NA MTOTO WANGU."

Alipoulizwa ni nani analala na Rayvanny, Fahima alijibu hivi.

"MFUATE YEYE UMUULIZE."Fahima Alisema.

Aliongeza na kusema kuwa ameacha kuwa video vixen. Fahima awali amekuwa video vixen kwa nyimbo mbili pekee ambazo ni za Rayvanny alikiri na kusema kuwa endapo Rayvanny anataka awe Video Vixen atamuitisha mamillioni ya pesa.

“I’M DONE BEING A VIDEO VIXEN AND IF ITS RAYVANNY’S VIDEO, I MIGHT DO IT BUT HE WILL PAY ALOT OF MONEY FOR ME TO LEAVE MY BUSINESSES AND DO THAT. IT IS BUSINESS AT THE END OF THE DAY.”

Matamshi ya Fahima yanakuja siku chache baada ya Rayvanny kutoa picha zake zote kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.