Muwe macho! Msiruhusu watu kutoka Tanzania kuvuka ovyo ovyo - Wamalwa asema

Waziri wa Ugatuzi nchini Eugene Wamalwa amesema ni rasmi kuwa sasa ongezeko la virusi vya corona vinavyoshuhudiwa nchini vinatokana na watu kuvuka mipaka ovyo ovyo na kuingia nchini kinyume na masharti.

Wamalwa amezitaka asasi za usalama wa kaunti ya Narok haswa katika mpaka wa Oloposimorum unaunganisha kenya na Tanzania kuwa ange na haswa kutowaruhusu watu kutoka kwa taifa hilo kuruhusiwa kuingia nchini.

Wamalwa amesema visa vya hivi karibuni vilivyoripotiwa katika kaunti ya Wajir vilitokea katika taifa jirani la Somalia baada ya wakaazi wa eneo hilo kwenda kuuza ng'ombe, hatua ambayo imelifanya gatuzi hilo kuwa na virusi hivyo.

Alikuwa akisema hayo alipokuwa katika kanisa la Katoliki la Nairegia Nkare ambapo alikuwa anagawa chakula kwa waathiriwa wa mafuriko kutoka Narok Mashariki.

Miongoni mwa watu wengine waliokuwa na Wamalwa na waziri wa Mazingira Keriako Tobiko na viongozi wengine wa kisiasa kutoka ukanda huo.

Watu wanne katika kaunti ya Narok wamepoteza maisha yao kutokana na mafuriko na wengine 6,000 kukosa makao baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko.