Mvulana mmoja mwenye miaka 13 ajitia kitanzi huko Busia

Mtoto mmoja mvulana mwenye umri wa miaka 13 kutoka kijiji cha Mung’ambo eneo bunge la Butula kaunti ya Busia amejitia kitanzi kwenye nyumba ya nduguye katika hali ya kutatanisha.

Kamanda wa polisi kaunti ya Busia John Nyoike amesema kuwa mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi katika moja mjini Busia na ambaye ni mtoto wa aliekuwa mwakilishi wa wadi ya elugulu na kiongozi wa wengi kwenye bunge la kwanza la kaunti ya Busia Josephat Wandera, alitoweka nyumbani kwao jana alasiri kabla ya kupatikana akiwa amejitia kitanzi juu ya paa ya nyumba hiyo.

Maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho.

Kwingineko

Zaidi ya familia 20 zimeachwa bila makao katika Kijiji Cha Ndovuni huko Maungu kaunti ya Taita Taveta kufuatia mafuriko.

Wakazi sasa wanaitaka serikali na makundi ya kutoa misaada kuwaidia baada ya nyumba zao kusombwa na maji ya mafuriko yanayodaiwa kutoka nyanda za juu milimani.

Wameitaka serikali ya kaunti pia kuimarisha kitengo Cha kukabili majanga.

Kwingineko

Almashauri ya kukusanya mali ambayo hajatwaliwa( Unclaimed Financial Assets Authority, UFAA) imezindua kampeni ya kuhamasisha wakazi wa kaunti za Taita Taveta, Kwale na Mombasa kuhusu jinsi ya Kupata mali zao zilizotwaliwa na mamlaka hiyo.

Mkurugenzi wa almashauri hiyo Thomas Mwadeghu anasema jumla ya shilingi milioni 400 kutoka kaunti hizo tatu bado hazipata wenyewe. Amewataka wakenya kutembelea tofuti ya UFAA ili kujua iwapo wanadai pesa.