Mvulana wa miaka 14 akamatwa kuhusiana na mauaji ya mwanahabari Kibra

gang
gang
Polisi wamemkamata mvulana mwenye umri wa miaka 14 kuhusiana na amuaji ya mtangzaji wa kituo cha redio cha Pamoja FM mtaani Kibra  Mohamed Marjan.

Mohamed  alipatikana ameuawa Mei tarehe 4 na mwili wake ukiwa barabarani eneo la Makina karibu na mahakama ya Kibera. Makachero wamemkata mshukiwa huyo baada ya kuitathmini kanda ya video yaa ya CCTV. Alikuwa akielekea nyumbani  alfajiri baada ya kufanya kipindi cha usiku cha ‘ Ukumbi wa Kiislamu’ 

Picha hiyo ya video ilimuonyesha mvulana huyo mwenye umri wa miaka 14 akiwa pamoja na watu wengine wane wanaoshukiwa kuwa majambazi  wanaohudumu katika mtaa huo wa mabanda. Polisi wanasema washukiwa hao walimshambulia marehemu akiwa anaenda nyumbani. Kundi hilo kisha lilimwibia  kabla ya kumdunga kisu kifuani na kumuua papo hapo.

Mshukiwa mmoja alivamiwa na  wananchi kabla ya kutoroka. Polisi wanaendelea kuwasaka washukiwa wengine  watatu na mwanamke anayeaminika kuwapa hifadhi washukiwa hao. Polisi wamesema  kwamba mshukiwa wa pili alikamatwa na ndiye aliyetambua majina ya wenzake. Marijan  alikuwa mwanahabari aliyejituma na alikuwa nguzo muhimu kuanzisha kituo hicho cha redio mwaka wa 2006.