Mwakilishi wa wadi ya Witeithie aachiliwa kwa dhamana ya elfu 20

HAMMER
HAMMER
Mwakilishi wa wadi ya  Witeithie Julius Taki  katika kaunti ya Kiambu  ambaye gari laki lenye picha ya naibu wa rais William Ruto akiwa amevalia sare ya kijeshi  ameshtakiwa kwa kuendesha gari lilisilofaa kuwa barabarani .

Taki  alifikishwa kortini jumanne  na kukabiliwa na shtaka la kuhudumu gari lilisolokuwa na mikanda ya usalama . mashtaka mengine yalikuwa ,kuwabeba abiria wengi kupita kiasi na kuwa vioo vyenye rangi . Alikana mashtaka hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi  20,000 pesa taslimu .

Hata hivyo uhuru wa Bwana Taki haukudumu kwani  upande wa mashtaka uliwasilisha ombi kutoka DCI kumzuilia ili kukamilisha uchunguzi kuhusu  alikotoa nembo za serikali zilizokuwa katika gari lake .  upande wa mashtaka  umeimbia korti kwamba polisi wanahitaji kufahamu zilikotolewa nembo hizo . mahakama ilikubali ombi lao na kesi hiyo itasikizwa  Juni tarehe nne .