Mwakilishi wa wanawake Baringo apoteza mumewe kutokana na Corona

Isaac
Isaac
Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Baringo Gladwell Tungo anaomboleza kifo cha mumewe  Isaac Cherogony ambaye alifariki kutokana na virusi vya corona akiwa katika hospitali Eldoret.

Kulingana na taarifa, Cherongony alifariki Jumamosi akipokea matibabu baada ya kuanza kuonyesha dalili za kushindwa kupumua na hivyo kukimbizwa katika hospitali na hatimaye kufariki.

Kutokana na tukio hilo, Tungo amefanyiwa vipimo kuhusiana na virusi hivyo na anatarajiwa kupokea matokeo yake wiki hii.

Boma lake sasa limewekwa chini ya uangalizi huku watu waliokuwa na mwathiriwa wakiendelea kutafutwa.