Mwalimu akana kumbaka na kumpachika mimba mwanafunzi wake

kimanthi
kimanthi
Mwalimu kutoka Embu aliyekisiwa kumdhulumu na kumpachika mimba mwanafunzi wake baada ya kuahidi kumlipia karo ya shule amefikishwa mahakamani.

Moses Kimanthi, ambaye ni mwalimu wa somo la kompyuta katika shule ya Muvandori Day Secondary School alikana mashtaka mbele ya hakimu mkuu Tony Kwambai.

Upande wa mashtaka ulisema alimdhulumu mwanafunzi katika tarehe tofauti kati ya Julai 7 na 23 mwaka jana.

Kimanthi anakabiliwa na shtaka mbadala la kugusa sehemu za siri za msichana huyo akitumia sehemu zake za siri katika mji wa Manyatta kata ndogo ya Embu kaskazini.

Wakili wa mtuhumiwa, Victor Adande aliiomba mahakama imwachilie kwa dhamana ili aweze kuhudhuria mahakama kutoka nyumbani.

Andande alisema mwalimu huyo ni mwanafunzi katika chuo Kikuu cha Mt Kenya na anahitaji wakati wa kuendelea na masomo. 

Kwambai alimwachilia mwalimu huyo kwa dhamana ya Sh100,000 na dhamana ya pesa ya Sh50,000. Kesi hiyo itaskizwa mnamo Machi 30. 

Yatima alisema baada ya kuahidi kwamba atamsaidia kumaliza deni la karo yake ya shule, mwalimu huyo alimkaribisha kwenye nyumba yake ya kukodisha huko Manyatta Town ambako walishiriki ngono.

Mlalamikaji alisema walishiriki ngono bila kinga kila Jumapili baadaye kabla ya kugundua kuwa alikuwa mjamzito na alimjulisha mwalimu.

Alisema mwalimu huyo alimtishia kwamba atamuua ikiwa atafichua kilichotokea.

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya kaskazini mwa Embu, Godfrey Kere alisema kuwa familia ya mwathiriwa iliripoti kisa hicho katika Kituo cha Polisi cha Kibugu na kupelekea kukamatwa kwa mwalimu huyo Jumatatu.

Kere alisema kuwa mama ya mlalamikaji aliripoti katika kituo cha polisi kwamba Kimanthi alimdanganya binti yake ili washiriki mapenzi naye na kumpachika mimba.