Mwalimu mmoja wa shule ya msingi ameuawa kwa kupigwa risasi ilhali maafisa wawili wa polisi wa utawala wamejeruhiwa baada ya gari la polisi kushambuliwa na majangili huko Turkana mashariki .kamanda wa polisi wa kautni ya Turkana Samuel Ndanyi amesema gari hilo la polisi lilikuwa likielekea katika kituo cha kibiashara cha Lokori kutoka Napeiton .
Shambulizi hilo lilitokea mwendo wa saa tatu unusu asubuhi . Mwalimu aliyeuawa ametambuliwa kama Oscar Keya ambaye alikuwa katika likizo ya katikati ya muhula na alikuwa ametumia usafairi wa gari hilo la polisi kwa sababu eneo hilo halina huduma za usafiri wa umma kwa ajili ya hali mbaya ya usalama na ubovu wa barabara .
Kamanada huyo wa polisi wa kaunti amesema maafisa wa GSU na RDU tayari wametumwa katika eneo hilo kuwasaka majangili waliotekeleza shambulizi hilo