Mwalimu mkuu amchapa hadi kumuua mwanawe kwa kuwa na mpenzi

9k=
9k=
Ni mambo ambayo anaendelea na yanazidi kutendeka haswa wakati huu wa janga la corona na wakati ambao wanafunzi wengi wamo nyumbani na wazazi wao.

Mwalimu mkuu wa shule ya upili alimchapa hadi kifo mwanawe wa miaka ,17, duru za habari zinaarifu kuwa alimfumania mwanawe kwa nyumba ya mpenzi wake, na kuanza kumchapa bali hakujua hawakukosea waliposema hasira hasara.

Mtoto huyo alikimbizwa katika hospitali ya Migori kupokea matibabu ya kwanza.

Mwalimu huyo aliyefahamika kama Abidha Rabet, kulingana na mashahidi ni mwalimu mkuu wa shule ya upili ya St Juliane Ugari, mwanamume aliyekuwa na mwanafunzi huyo alitoroka baada ya kuona kisa hicho.

Jamaa za Rabet walichukuwa mwili wa mwendazake na kutaka kuuzika bali polisi waliingilia kati, mkuu wa polisi wa kaunti ndogo ya Uriri  Peter Njoroge alithibitisha kisa hicho na alikuwa na haya ya kusema,

“We coordinated with police manning a roadblock in Homa Bay town and intercepted the vehicle which was heading to Bond. They intended to inter the body secretly." Alizungumza Njoroge.

Mwili wa mwendazake ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha St Joseph Onbo, huku polisi wakizidi kufanya uchunguzi na kubaini nini kilichosababisha kifo cha mwanafunzi huyo.

Kwa kweli Unyama umetoka kwa wanayama na kuwaingia wanadamu, mshukiwa kwa sasa yuko mikononi mwa polisi uchunguzi unapoendelea.